Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani hufanyika Mei 1, kila mwaka Duniani kote kwa lengo la kuwakumbuka na kutambua mchango wa wafanyakazi katika kuleta ustawi na tija katika sekta mbalimbali.

Wafanyakazi wamekuwa nguzo muhimu katika kujenga uchumi imara na kuongeza uzalishaji, huduma bora na mwelekeo chanya katika sekta zote.

Ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa Mei Mosi mwaka huu wa 2026 mjini Njombe ni kuwathamini na kutambua mchango wa Wafanyakazi hapa nchini, kauli hii imekuja wakati muafaka, sambamba na hatua kadhaa alizochukua katika kuboresha mazingira na maslahi ya watumishi.

Tunayo kila sababu ya kupongeza jitihada hizi za kuwawezesha wafanyakazi ikiwemo kulipa madeni, kupandisha kima cha chini kwenye sekta binafsi, kuboresha mazingira ya kazi, kutoa maelfu ya ajira kwa watanzania na pia kuweka mkazo katika kujenga mazingira bora ya kazi.

Hongera Mhe. Rais kwa kazi hii njema, Wafanyakazi wako nyuma yako na tunaahidi kuendelea kuchapa kazi.