Amani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa letu. Kwa Watanzania, amani haiishi serikalini pekee, bali iko ndani ya mioyo yetu. Tumeishi kwa amani kwa miongo mingi, tukizoea na kuipenda nchi yetu. Watanzania ni watu wavumilivu, wenye hekima na wasioyumbishwa kwa urahisi na masuala ya chokochoko au uchochezi.
Tofauti zetu za kisiasa, kiuchumi au kijamii zinaweza kurekebishwa kupitia mazungumzo ya busara na maelewano, badala ya kufanya vurugu, tujadiliane na kuridhiana kama tulivyofanya tangu uhuru wetu. Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuleta maendeleo katika sekta zote, hivyo ni wajibu wetu sisi wananchi kuilinda amani hii ili tuendelee kujenga taifa lililo imara.
Nawaomba ndugu zangu Watanzania, tukatae kabisa uchochezi wa baadhi ya wanaharakati na watu wasiopenda amani ambao wanataka kuvuruga utulivu wetu kwa lengo la maslahi binafsi. Amani yetu ni hazina kubwa ambayo haiwezi kubadilishwa na maneno ya chuki au propaganda za mitandaoni.
Tushikane mikono, tuunge mkono juhudi za serikali na kuendeleza umoja wetu. Tuwe macho na tuwaripoti wale wanaotaka kuharibu amani. Tanzania yetu iendelee kuwa kisiwa cha amani katika Afrika na duniani kote.
Amani ni uhuru, Amani ni maendeleo!